KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Tuesday, July 17, 2012

JIJI LA MBEYA LAPOKEA INJIILI KWA UPYA


Na:Yonathan Landa.
NGUVU YA MAOMBI YATIKISA WANAWAKE WA JIJI LA MBEYA.
WANAWAKE WA INJILI (WWI) WA KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA JIMBO LA MBEYA WASEMA SASA TUMEPONA!
Zilikuwa ni siku tano za aina yake katika Jiji la Mbeya na vitongoji vyake wakati kongamano kubwa la wanawake wa kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania jimbo la Mbeya walipokusanyika katika Kanisa la EAGT Gilgali Mwanjelwa linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Dr. Asumwisye Mwaisabila ambaye pia ni Makamu wa Askofu Mkuu Tanzania.

Blog hii nayo ilikuwa ni miongoni mwa waliohudhulia toka mwanzo wa Kongamano hilo lililoanza siku ya Jumanne ya tarehe  03 july 2012 hadi siku ya jumamosi ya tarehe 07 july 2012 hitimisho lake katika siku tano mfululizo, Ambapo mtumishi wa Mungu Mchungaji Florian Katunzi wa Kanisa la EAGT City Center alikuwa ni Mwalimu wa kongamano hilo toka inje ya mkoa wa Mbeya.
Hakika Mungu alimtumia kwa ufasaha kufundisha somo la MAOMBI NDANI MWA MAOMBI, somo ambalo alisema limejengwa katika njia kuu tatu.
1.      Njia ya kwanza ni kuanza katika maombi.
2.      Njia ya pili kudumu katika maombi.
3.      Njia ya tatu kumaliza katika maombi
Mchungaji Katunzi amesema kuwa Huu ni wakati wa mkristo kuomba na si wakati wa mkristo  kulala usingizi , kwani  mkristo asiyeoomba hawezi kushindana na nguvu zozote zile za giza.
Akifundisha kwa hisia kali na uchungu moyoni Mchungaji Katunzi alisema kuwa Kanisa waliloanza nalo akina Moses Kulola na Asumwisye Mwaisabila walianza katika hali maombi na wakadumu katika hali ya maombi, tofauti na Kanisa la sasa ambalo halijadumu katika hali maombi na matokeo yake Wakrito wengi hawana nguvu za Mungu zipatikanazo ndani ya maombi hayo.
Akifafanua baadhi ya Maandiko Matakatifu Mchungaji Katunzi amesema kuwa wakati Mtume Petro alipofungwa gerezani na Mfalme Herode Kanisa la wakati ule lilisimama kidete na likaomba kwa bidii sana, na hata milango ya gereza ikafunguka na hatimaye Petro alitoka Ndani ya gerezakwa mkono wa Mungu wenye nguvu, Matendo ya Mitume 12:1.

Hivyo tunapoombea Ndoa zetu,ni lazima zile Ndoa zilizomo gerezani zifunguke, biashara zilizopo gerezani zifunguke,ila ni pale tu! tutakapoomba kwa bidii, Hivyo mwanamke wa injili simama uombe kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya watoto wetu,na kwa ajili ya mali zetu na waume zetu pia, Ni maombi pekee ndiyo yanayofungua njia iliyonyooka kwa muombaji  Ezra 8:21 – 23, Hivyo usipuuze maombi mwana wa Mungu maana utakapoomba kwa bidii utapewa sawa sawa na maombi na sio nje ya maombi, Zaburi 20:8, hivyo wamama wa injili kuweni kama wanawake wa Biblia ambao waliomba pasipo kuchoka, nanyi mtavuna msipozimia roho maana maombi hayafi.
Katika siku ya mwisho ya kongamano hilo Mchungaji Katunzi alihitimsha kwa maombi maalumu ya Baraka za kifamilia na ulinzi wa ukuta wa moto ambapo alitamka Baraka maalumu kwa wote waliofika katika kongamano hilo kwa kuwaombea ustawi wa kiroho na kimwili pamoja na ustawi wa watoto wao na waume zao pia.
Wakizunguza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake waliofika katika kongamo hilo wamesema kuwa hakika kongamano hili limekuwa la Baraka sana kwetu sisi akina mama wa Mbeya kwani sasa Kanisa la mkoa wa Mbeya limepata nguvu mpya na Ndoa zetu zimepo kabisa na watoto wetu nao wamepona na hata mali zetu pia zimepona kwelikweli.
Naye Mkurugenzi wa wamama wa jimbo la Mbeya Mama Mchungaji Mlawa amesema huu ni wakati ambao Bwana Yesu alikuwa ameukusudia kwetu na hakika Mungu amemtumia mchungaji Katunzi sawasawa na vile ambavyo sisi wamama tulimuomba Mungu ampe Ujumbe Mchungaji Katunzi wakusema nasi wamama na kweli hii inadhirisha wazi kongamo hili lilikuwa na nguvu zisizo za kawaida na Mungu ameongea nasi.

Aidha kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa Kanisa EAGT Gilgali Mwanjelwa Makamu Askofu Mkuu Dr. Asumwisye Mwaisabila yeye amasema kuwa Mchungaji Katunzi amefanyika Baraka katika kongamano la wamama na hakika ameona Mungu akimtumia kwa namna ya ajabu sana na akamuonya akisema kuwa kamwe asije akaacha injili anayohubiri sasa kwani  Bwana Yesu  amemuitia injili hiyo, na mwisho Askofu Dr. Mwaisabila akatoa nasaha zake akisema  “Mwanangu Katunzi huu  si muda wa kusikiliza maneno ya watu kwani hayana maana katika kazi Bwana wetu Yesu Kristo mimi Baba yako Nakupenda sana furaha yangu ni wewe kusonga mbele, Na kama mimi Baba yako ningelisikiliza Maneno ya watu nisingefika hapa nilipofika, hivyo Mwanangu Katunzi songa mbele kwa kazi ya Bwana Yesu mimi ni Mzee sasa nataka twende Mbinguni Kijana wangu  ” hayo ni maneno ya wosia ya Askofu Mwaisabila aliyoyatoa kwa mchungaji Katunzi ambapo watu wote waliokuwepo ndani ya kongamano hilo walishindwa kujizuia na kupelekea kuangua kilio kikubwa kilichotikisa kongamano zima kwa maneno mazito ya Mzee huyu.
Kwa upande wake Mchungaji Katunzi yeye alifurahishwa kwa namna ambavyo Mungu alivyoonekana katika wiki yote ya Kongamano la wamama na zaidi aliwashukuru wamama wote wa Mji wa mbeya kwa namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe wake wote, “Kwa kweli ninyi akina mama mmekuwa chachu ya injili kila mahali injili inapofika hakika ninyi ni jeshi kubwa sana, na kipekee nimshukuru Makamu Askofu Mkuu Dr. Mwaisabila na Timu yake ya hapa Mbeya kwa kuweza kuratibu vema kongamano,kwa ushirika mkuu na Ofisi ya Jimbo la Mbeya”
Mwisho Mchungaji Katunzi alitoa Mchango wa Fedha shilingi laki tano kwa wamama wa Jimbo la Mbeya ambayo aliwakabidhi viongozi wajimbo hilo kwa niaba ya wamama wote,  huku Madhabahu ya Kanisa la EAGT Gilgali Mwanjelwa akiichangia kiasi cha Fedha Shilingi laki tano ambapo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Makamu Askofu Mkuu Dr. Mwaisabila alikabidhiwa na Mchungaji Katunzi.  

Picha ya chini ni Mchungaji Athanase Camilly akifundisha katika kambi la wamama mjini Mbeya.

 Akina Mama wakiomba kwa bidii katika kongamano laWWI Mbeya mjini.
 Mchungaji Katunzi akitoa Mchango wa Shilingi laki tano kwa viongozi wa WWI Mbeya.
 Mchungaji Katunzi akongoza Maombi kwa wamama pamoja na picha zinazofuata hapa chini.



 Makamu wa Askofu Mkuu wa EAGT Dk. Asumwisye Mwaisabila akongea na Wamama.
 Askofu Mwaisabila na Mchungaji Katunzi wakieleza jambo kwa pamoja katika Kongamano hilo.
 Askofu Mwaisabila akimuombea Baraka Mchungaji Katunzi na Ulinzi wa Mungu.
 Askofu Mwaisabila na Mchungaji Katunzi akikumbatiana kwa Furaha baada ya Kongamano kumalizika.

No comments:

Post a Comment