KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Wednesday, July 18, 2012

WAZO LA MUNGU LILIVYOFANIKIWA MBEYA


Na Yonathan Landa.
Kanisa la Tanzania Assemblies Of God Mkoa wa Mbeya limefanya Semina ya Nguvu za Mungu yenye kichwa cha somo WAZO LA MUNGU  kwa Ushirikiano wa Makanisa matano kwa ajili ya kuharibu kazi za shetani mkoani hapo, Kanisa hilo ambalo ni moja kati ya makanisa yaliyojitolea kupelekea injili ya Kristo Yesu mwana wa Mungu kwa gharama wamefanya semina hiyo kuanzia siku ya Jumatano ya tarehe 11 July 2012 hadi siku ya Jumapili ya tarehe 15 July 2012 katika Kanisa la TAG – Rehoboth International Christian Center (RICC) linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Sunday Matondo ambaye ndiye aliyekuwa  mwenyeji wa Semina hiyo.
Semina hiyo ambayo ilihudhuriwa na waumini mbalimbali kutoka makanisa mbalimbali hakika ilikuwa na nguvu za Mungu zisizo za kawaida hasa kutokana na watumishi waliokuwa wakiendesha semina hiyo kuwa na Nguvu za Mungu zisizo za kawaida.
Semina hiyo ilifundishwa na wahubiri kutoka ndani ya nchi yetu ya Tanzania na kutoka nchi jirani ya Malawi ambapo kutoka Tanzania Mchungaji Frolia Katunzi kutoka Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania alifundisha na kutoka Malawi alifundisha Askofu na Nabii  Steven Mwila, huku wachungaji wenyeji walioshiriki kuratibu semina nzima ni Mchungaji Lauden Mwafongo kutoka TAG – Gilgali RRM na Mchungaji Imani Masiku kutoka TAG – Jorai  Itunda.

Katika picha ni baadhi ya matukio yaliyoweza kupatikana na Kamera yetu.

 Picha juu ni Kanisa la Rehoboth International Christian Center TAG uso wa mbele.
 Picha ya Juu ni Baadhi ya Wachungaji washiriki katika Semina ya Wazo la Mungu.
 Askofu na Mtume Steven Mwila na Mkewe wakifuatilia kwa makini wakati Mchungaji Katunzi alipokuwa akifundisha.
 Meneja wa Radio Ushindi Mchungaji Mathew Sasali iliyoko Mkoani Mbeya akifuatilia kwa Makini mafundisho ya Wazo la Mungu.
 Mchungaji Katunzi wa Kanisa la EAGT City Center akiendesha Maombi huku Mchungaji Sasali akiendesha Timu ya Kusifu na Kuabudu.
 Mchungaji Mwenyeji Sunday Matondo na Askofu na Nabii Mwila wakiwa wamezama katika hali ya Maombi kwenye Semina ya Wazo la Mungu.
 Mchungaji Athanase Camilly wa EAGT Issanga Mbeya akiwa amezama kwenye Maombi na wachungaji baadhi.
 Haikuwa rahisi kwani hata waimbaji nao walizama katika hali ya Maombi kama unavyoowaona.


 Picha tatu za Juu ni Mchungaji Katunzi akiendesha Maombi kwa baadhi ya washiriki wa semina ya Wazo la Mungu.

No comments:

Post a Comment