KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Friday, July 27, 2012

SEMINA YA KKKT KURASINI NA MWINJLISTI KIUNGO


Picha ya juu Mchungaji Dk. Ngaleni akimkaribisha Mhubiri wa Semina Mwinjilisti Kiungo tayari kwa Neno la Semina.
Picha ya juu ni Mwinjilisti Kiungo akisalimia Wanasemina Katika Kanisa la KKKT Kurasini hapo jana.
 Picha ya juu ni Mwinjilisti Kiungo akiongoza kipindi cha kumuabudu Mungu kabla ya neno.
 Picha ya juu ni baadhi ya Washiriki wa semina katika Kanisa la kurasini wakimuabudu Mungu kwa pamoja.
 Picha ya juu ni baadhi ya washiriki waliofika kwenye semina wakimuabudu Mungu kabla yaNeno.
 Picha ya juu ni Mchungaji Dk. Ngaleni akimuabudu Mungu kabla ya Neno la Mungu.

 Picha ya juu ni Bango la kitambaa likionekana mbele ya Kanisa na Ujumbe wa Semina.
 Picha ya juu ni baadhi ya waimbaji wakishiriki kwa pamoja katika kumuabudu Mungu.

 Picha juu ni Mwinjilisti Kiungo akifungua kwa maombi semina ya Neno la Mungu yenye kichwa cha somo Mtakatifu ni Nani.



Hapa chini ni Mafundisho ya Semina ya leo.

      MAMBO YA MUHIMU UKITAKA KUWA MTAKATIFU
Nini maana ya utakatifu?
1.    Utakatifu maana yake ni kuwa mkamilifu.
 Mt.5:48. “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu,  kama Baba yenu wa Mbinguni alivyo makamilifu .”
Law.11:44; “ Kwakuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu;takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwakuwa mimi ni mtakatifu;  wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya Nchi.”
Law. 19:2; “Nena na mkutano wote wa wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA Mungu wenu, ni mtakatifu.”
Law. 20:7,26 “Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu, nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.”
2.    Mtu asiye na hatia.
 Efe.1:4 “Kama vile alivyo tuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”
MAISHA YA MWANADAMU KABLA YA DHAMBI
MWA. 2:4-18, 21-25 “ Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na Nchi hapa kuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi.   Ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani  pumzi ya uhai akawa nafsi hai. BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.  BWANA Mungu akachipusha kila  mti unaotamanika kwa macho, na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Ukatoka mto katika Edeni na kuitilia bustani maji na kutokea hapo ukagawanyika ukawa vichwa vinne. Jina la wa kwanza ni Pishoni, na ndio unaozunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu; na dhahabu ya nchi ile ni njema;huko kuna bedola na vito Shoham.  Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. Na jina la mto wa tatu ni Hedekeli, ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wan ne ni Frati. BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi  wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapo kula matunda ya mti huo utakufa hakika. 18. BWANA Mungu akasema si vema mtu huyo awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 21-25. BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kasha akatwaa ubavu wake mmoja kafunika nyama mahali pake. Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke
ASILI YA MWANADAMU MDHAMBI
Angalia mwanzo wa dhambi ilivyoingia
sasa uk ifika sura ya nne Adamu na mkewe wanaanza kupata watoto, wakiwa nje ya bustani ya Edeni- angalia watoto wanazaliwa
Mwa. 3: 1-19,22-24- “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke,at! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, matunda ya miti ya bustani twaweza kula;lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayo kula matunda ya mti huo, mtafumbuluwa macho,  nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula wapendeza macho nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mmewe naye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua ya kuwa wa uchi wakashona majani ya mtini wakajifanyia nguo. Kasha wakasikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adam na mnkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adam akasema uko wapi? Akasema  nalisikia sauti yako bustanini nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi, nikajificha. Akasema ninani aliye kuambia ya kuwa uuchi? Je umekula wewe matunda ya  mti niyo kuagiza usiyale? Adamu akasema huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja name ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya nikala. BWANA Mungu akamwambia nyoka kwasababu umefanya hayo, umelaaniwa kuliko wanyama wote , na kuliko  hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wake na uzao wako; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino.  Akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tama yako itakiwa kwa mmeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza nikisema usiyale, ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapo irudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u m avumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”
, roho ya ukaidi inaendelea- Kaini anamuua Abeli-wivu
Mwa.4:1-15 “Adamu akamjua mkewe naye akapata mimba, akazaa kaini akasema, nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi sadaka  kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona  za wanyama. BWANA akamtakabari Habiri na sadaka yake; bali kaini hakumtakabari wala sadaka yake. Kaini akagadhabika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, kwa nini unaghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vema hutapata kibali?usipotenda vyema dhambi iko, ina kuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, ( twende uwandani)  ikawa walipo  kuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.  BWANA akamwambia Kaini yuko wapi Habili ndugu yako? Sijui, mimi nimlinzi wa ndugu yangu? Akasema umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapo ilima ardhi haitakupa mazao yake;  utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.  Kaini akamwambia BWANA,adhabu yangu imenikulia kubwa haichukuliki. Tazama umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, name nitakuwa mtoro na mtu asiye kikao duniani, hata itakuwa kila anionaye ataniua. BWANA akamwambia, kwa sababu hiyo yeyote atakaye mwua Kaini atapatilizwa kisasi mara saba, BWANA akamtia Kaini alama mtu amwonaye asije akampiga.”
- mjukuu wa Kaini anaoa mitala kwa mara ya kwanza
Mstari wa 19 “ Lameki akajitwalia wake wawili; jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.
Mstari wa 25-26-kwa mara ya kwanza watu walianza kuliitia jina la Bwana
Mwa. 5:24 – Hapa tena tuna muona Henoko anakwenda pamoja na Mungu
Mwa. 6-9- Mungu alichoka na maisha ya mwanadamu akaamua kuangamiza.
Huwo wote ni mfululizo wa maisha ya watenda dhambi ndiyo sababu ya Daudi kusema maneno yafuatayo
 Zab. 51:5 “ Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama alinichukuwa mimba hatiani.”
Ayu. 14:4 “ Ninani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.”
Rum.5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.”
Mwa. 5:3  “ Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake , akamwita jina lake Sethi.”

Nani mtakatifu?
1Yoh. 1:8-9 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu,  na kutusafisha na udhalimu wote.”
Mith.28:13 “ Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
MAMBO AMBAYO NI LAZIMA UFANYE ILI UWE MTAKATIFU
KUZALIWA MARA YA PILI
Yon. 3:1-6 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa wayahudi. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hapana mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu akamwambia amini, amini nakuambia, mtu asipo zaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, awezaje, mtu kuzaliwa akiwa mzee? Awezaje kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili , akazaliwa? Yesu akajibu amini, amini nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”
Eze.36:25-27 “ Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uovu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.  Name nitawapa ninyi moyo mpya, name nitatia roho mpya ndani yenu, name nitatoa moyo wa jiwe uliyomo ndani ya  mwili mwenu,name nitawapa moyo wa nyama. Name nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwa endesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”
Tit.3:5 “ Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyo yatenda sisi, bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.”


KUSAMEHE
Mt.6:14-15 “ Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na baba yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Mk.11:25-26 “ Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni mkiwa na neno juu ya mtu; ili na baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala baba yenu aliye mbinguni, hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Mt.5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni na huku ukikumbuka kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi utoe sadaka yako.”

KUTOA  SADAKA
               AINA ZA MATOLEO.

 

1      LIMBUKO (Malimbuko): Mith 3:9-10

v Limbuko ni zao la kwanza la kazi ya mikono yako. (First fruits)
·       Kazi ya limbuko, ni kumheshimu Mungu

3.    ZAKA ( FUNGU LA KUMI):  Walawi 27:30, Malaki 3:7 – 7
Mwanzo wa zaka
Zaka ilianza zamani kabla Mungu hajaweka sheria ya watu kutoa zaka. Wako watu walio mpenda Mungu kwa mioyo yao na walio mtolea Mungu bila kulazimishwa na sheria ila walitoa kwa mioyo yako. Watu hawa walitoa aina hii ya sadaka ikamfurahisha Mungu kiasi ambacho alivyo barikiwa nayo akaamua kuweka sheria ili vizazi vyote duniani vifute sheria hii kwa ajili ya kujipatia Baraka. Angalia mifano ifuatayo ni ya watu wa kwanza walio toa sadaka hii ya zaka kabla ya sheria ya Musa.
v IBRAHIM Mwa.14: 17-20 : “ Abrahamu aliporudi kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfale wa Sodoma akatoka amlaki katika Bonde la Shawe, nalo ni bonde la mfalme. Na Melkizedeki mfalme wa Salem , akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana.  Akambariki, akasema, Abrahamu na abarikiwe na Mungu aliye juu sana, muumba mbingu na Nchi.  Ahimidiwe Mungu aliye juu sana,  aliye watia adui zako mikononi mwako. Abram akampa fungu la kumi la vitu vyote.”
v YAKOBO Mwa. 28: 20-22 “ Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja name, akinilinda katika njia niiendayo na kunipa chakula nile, na nguo nivae,  name nikirudi kwa amani nyumbani kwa Baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililo lisimamisha katika nguzo  litakuwa nyumba ya Mungu wangu. Na katika kila utalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”


-   Zaka ni 10% (asilimia kumi) au 1/10 au sehemu moja kati ya kumi ya baraka yoyote aliyokupa Mungu.
 “lete zaka kamili nyumbani kwangu” (Malaki 3:10)
v Kazi ya zaka – ni kufungua madirisha ya mbinguni ili baraka zimiminwe.  Zaka haipimi baraka (mavuno) bali inafungua madirisha ya mbinguni ili upimiwe baraka kutoka kwenye matoleo ya sadaka yako baada ya zaka.
·       Endapo utazidiwa  na matumizi, na ikakulazimu kuitumia zaka takatifu ya Mungu, fahamu kwamba, Mungu anakudai.  Siku utakapomrudishia,  utatakiwa kulipa pamoja na riba, ili zaka yako ikombolewe.

·       Kukombolewa maana yake ili iwe zaka takatifu tena  ni lazima uiongezee 20% au 1/5  (sehemu ya tano )ya hiyo zaka, iwe kama riba, ndipo Mungu ataipokea kuwa ni zaka takatifu ya Bwana.  Laa sivyo, zaka yako, si kamili, hivyo si takatifu.  Kwahiyo, haitafungua madirisha ya mbinguni.

3.                                                                DHABIHU (Sadaka ya kawaida)   *2Kor 9:6-7
·       Sadaka ya dhabihu haina hesabu toka kwa Mungu, bali kila mtoaji, anaamua mwenyewe atoe kiasi gani.  Utakavyoamua ndivyo utakavyovuna.  Ukitoa kidogo,utavuna au utapimiwa kidogo, ukitoa kwa wingi, utapimiwa vingi. Ni uamuzi wako. (Gal 6:7 – 10)
·       Kazi ya Dhabihu: Ni kupima kiwango cha mavuno ya baraka, unayotakiwa kumiminiwa kutoka mbinguni baada ya kutoa zaka.


UONGOZWE NA ROHO MTAKATIFU
Mwa. 1:1-2 “ Hapo mwanzo Mungu aliziuumba mbingu na Nchi. Nayo Nchi ilikuwa ukiwa tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Mdo. 1:8 “ Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa Nchi.”
Rum.8:1-11 “ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria,  kwa vile ilivyo dhaifu kwasababu ya mwili, wangu,  kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.  Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa  Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu I hai kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliye mfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anaye kaa ndani yenu.”
Kwa hiyo ili mwadamu akamilike hatu tatu muhimu lazima zipitiwe
v MUNGU BABA- yeye ndiye muumbaji                  - lazima aumbe
v MUNGU MWANA- yeye ndiye mkombozi           - lazima aokoe
v MUNGU ROHO MTAKATIFU- yeye ni mtakatifu  - lazima atakase
BY EV. TITUS G. KIUNGO (titus2tz@yahoo.co.tz) facebook- titus kiungo

No comments:

Post a Comment