KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Friday, September 21, 2012

WAKATOLIKI KUWENI WAFIA DINI

Na Gazaeti la Kiongozi.
Askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Dodoma mhashamu Mathias Isuja amewataka watawa na waamini kwa jumla, kushikilia imani yao na kulinda huku wakimshuhudia Yesu hata kama wanakumbana na vikwazo vinavyowawezesha kukatwa shingo kwani wao ni wafiadini duniani wenye tunu mbinguni.

Amesema maisha ya utawa ni kufia dunia na kuishi hai kimungu hivyo, lazima waamini wakiwamo watawa kukubali kufia dunia kwa kujikatalia  kila kitu na kujitwika msalaba na hatimaye kumfuata Kristo. Askofu amesema hayo wakati akitoa salamu baada ya ibada ya jubilei ya miaka 25 na 50 ya masista wa shirika la mtakatifu jimboni Kondoa na kusisitiza kuwa, waamini wanapaswa kuona fahari ya msalaba kwakuwa ndani yake, kuna wokovu na raha ya milele.....






Askofu mstaafu Mathias Isuja akiwa na waziri mkuu mh. Mizengo Pinda.

No comments:

Post a Comment