KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Friday, October 19, 2012

WAISLAM VITANI NA JESHI LA POLISI

Leo katika Mitaa ya Jijini la Dar es Salaam hasa maeneo ya Kariakoo, Posta, na Kinondoni yalipo Makao Makuu ya Baraza la Kiislamu Tanzania BAKWATA yamekuwa na hali ya Sintofahamu kwa nyakati tofauti kutokana na Maandamano yaliyo hamasishwa na Baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu kwa lengo la kushinikiza kutolewa kwa Kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu Issa Ponda ambaye amefikishwa katika mkono wa sheria hapo juzi.
Waislamu baadhi walionekana wakirandaranda katika maeneo tajwa kwa lengo la wao kufanya maandamo yatakayoweza kushinikiza kutolewa kwa Bwana Ponda na wafuasi wake wapatao arobaini na tisa, lengo la maandamano hayo lilisikika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam baada ya Sala ya Ijumaa kumalizika.
Katika picha chini ni Baadhi za matukio yaliyojiri katika Jiji la Dar es Salaam.

 Jeshi la Polisi likiwa Makini kwa Hali yoyote katika Maeneo ya Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 Jeshi la Polisi wakiwa wamewakamata baadhi ya Waislamu walioandamana kupinga kwa kukamatwa kwa Kiongozi wao Ponda.

 Baadhi ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakitakiwa kuondoka katika eneo la Uzio wa Jeshi la Polisi maeneo ya Posta.

 Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) likiwa Makini kwa Hali yoyoteitakayotokea endapo Jeshi la Polisi watazidiwa Nguvu katika Maeneo ya Kariakoo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) likiwa Makini kwa Hali yoyoteitakayotokea endapo Jeshi la Polisi watazidiwa Nguvu katika Maeneo ya Kariakoo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 Baadhi ya waandamanaji walikamatwa na Jeshi la Polisi katika Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakipelekwa katika Kituo cha Polisi kilichopo Msimbazi.
 Baadhi ya waandamanaji walipigwa na Jeshi la Polisi katika Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakipelekwa katika Kituo cha Polisi kilichopo Msimbazi.

No comments:

Post a Comment