KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Thursday, November 8, 2012

NMB YAONGOZA KWA TUZO ZA WALIPA KODI NCHINI


 
Makamu wa Rais, Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja ya tuzo ya mshindi wa jumla kitaifa wa mlipa kodi hapa nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing kwenye hafla ya 6 ya Siku ya Mlipa Kodi jijini Dar es Salaam jana.
 
Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya NMB, Bw.Waziri Barnabas akiwa amebeba moja ya tuzo zilizokakabidhiwa kwa benki NMB baada ya kuibuka mshindi katika Siku ya Mlipa Kodi nchini. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. NMB ilikabidhiwa tuzo ya mshindi wa jumla kitaifa wa mlipa kodi, mshindi wa pili katika taasisi za fedha na mshindi wa pili katika kundi la walipa kodi wakuu nchini.
 
Makamu wa Rais, Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto kwake), Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing (Wa kwanza Kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Wa pili kushoto) Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya  (kushoto) na washindi kumi bora wa siku ya mlipa kodi nchini.

No comments:

Post a Comment