KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Monday, March 19, 2012

IBADA YA TAREHE 24 - 25 MARCH EAGT CITY CENTER

Na Yonathan Landa.
Dar es Salaam.
Jumamosi ya tarehe 24 jumapili ya tarehe 25 mwezi huu kutakuwa na ibada ya Mabinti wasioolewa wala kupata wachumba na Vijana ambao hajaoa wala kupata wachumba katika kanisa la EAGT City Cente kwa Mchungaji Florian Katunzi kanisac lililo katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere zamani Sabasaba.

Mchungaji Katunzi ameyasema hayo katika ibada ya Jumapili ya tarehe 18 mwezi huu, Mchungaji Katunzi amesema huu si wakati wa kutegemea zaidi kuombewa bila ya Mhitaji kumshii Mungu katika shida zake kwani kwa kutokufanya hivyo kutasababisha maangamizi mengi kutokea katika maisha ya vijana.

hivyo amewaomba Vijana kwa bidii yote waje katika maombi ya Tarehe 24 na 25 mwezi huu katika kanisa la EAGT City Center kwa Maombezi zaidi kwani hii ndio njia salama ya kukimbilia, aidha amegusia kwa wale wenye nyumba ndogo nao pia ni wakati wao wa kuweza kuachana na nyumba ndogo na kumrudia mungu ili aweze kuwapatia wenzi wao wa maisha katika njia iliyo halali ya kimungu.

amesema kuwa ibada hiiyo itakuwa na nguvu zaMungu zisizo za kawaida kwani Bwana Yesu atatenda Kazi iliyo Kuu kwa watu wake wa jiji la Dar es salaam. amewakumbusha wakazi wajiji hili na Mikoa ya jirani kutokusahau ya kuwa matumizi ya vitambaa na maji ya upako na vitu vinavyofanana na hivyo si salama katika maisha ya Kiroho na kimwili pia,

ameleezea na kufafanua kuwa amekuwa na wakati mwingi wa kufanya maombi na watu wanaofika kanisani kwake wakiwa na malalamiko ya kutokupata msaada walioutarajia katika Vitambaa, Maji ya Upako, Mafuta ya Upako, Chumvi, Sabuni ya Upako, hivyo anao ushahidi wa wazi juu ya Mengi katika hayo.

Picha za Chini Mchungaji Katunzi katika Ibada ya Jumapili ya tarehe 18 March mwaka huu.

No comments:

Post a Comment