Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi
wengine wakipata maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama
juu ya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu na vitega uchumi wa chama
hicho mjini Dodoma ambako alisimama kwa muda siku ya Jumanne Novemba 6,
2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo
juu ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa ‘White House’ ulio katika
makao makuu ya CCM mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili
kukidhi mahitaji ya sasa. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma
siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19
ndani ya wiki moja.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio
kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini
Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi
mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya
miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mafundi
rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi utaotumika wakati wa
mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment