Na:Yonathan
Landa.
NGUVU YA
MAOMBI YATIKISA WANAWAKE WA JIJI LA MBEYA.
WANAWAKE WA
INJILI (WWI) WA KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA JIMBO LA
MBEYA WASEMA SASA TUMEPONA!
Zilikuwa
ni siku tano za aina yake katika Jiji la Mbeya na vitongoji vyake wakati
kongamano kubwa la wanawake wa kanisa la Evangelistic Assemblies Of God
Tanzania jimbo la Mbeya walipokusanyika katika Kanisa la EAGT Gilgali Mwanjelwa
linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Dr. Asumwisye Mwaisabila ambaye pia ni
Makamu wa Askofu Mkuu Tanzania.
Blog hii nayo ilikuwa ni miongoni mwa waliohudhulia toka mwanzo wa
Kongamano hilo lililoanza siku ya Jumanne ya tarehe 03 july 2012 hadi siku ya jumamosi ya tarehe
07 july 2012 hitimisho lake katika siku tano mfululizo, Ambapo mtumishi wa
Mungu Mchungaji Florian Katunzi wa Kanisa la EAGT City Center alikuwa ni
Mwalimu wa kongamano hilo toka inje ya mkoa wa Mbeya.
Hakika
Mungu alimtumia kwa ufasaha kufundisha somo la MAOMBI NDANI MWA MAOMBI, somo ambalo
alisema limejengwa katika njia kuu tatu.
1. Njia ya
kwanza ni kuanza katika maombi.
2. Njia ya pili
kudumu katika maombi.
3. Njia ya tatu
kumaliza katika maombi
Mchungaji
Katunzi amesema kuwa Huu ni wakati wa mkristo kuomba na si wakati wa
mkristo kulala usingizi , kwani mkristo asiyeoomba hawezi kushindana na nguvu
zozote zile za giza.
Akifundisha
kwa hisia kali na uchungu moyoni Mchungaji Katunzi alisema kuwa Kanisa
waliloanza nalo akina Moses Kulola na Asumwisye Mwaisabila walianza katika hali
maombi na wakadumu katika hali ya maombi, tofauti na Kanisa la sasa ambalo halijadumu
katika hali maombi na matokeo yake Wakrito wengi hawana nguvu za Mungu
zipatikanazo ndani ya maombi hayo.
Akifafanua
baadhi ya Maandiko Matakatifu Mchungaji Katunzi amesema kuwa wakati Mtume Petro
alipofungwa gerezani na Mfalme Herode Kanisa la wakati ule lilisimama kidete na
likaomba kwa bidii sana, na hata milango ya gereza ikafunguka na hatimaye Petro
alitoka Ndani ya gerezakwa mkono wa Mungu wenye nguvu, Matendo ya Mitume 12:1.
Hivyo
tunapoombea Ndoa zetu,ni lazima zile Ndoa zilizomo gerezani zifunguke, biashara
zilizopo gerezani zifunguke,ila ni pale tu! tutakapoomba kwa bidii, Hivyo
mwanamke wa injili simama uombe kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya watoto
wetu,na kwa ajili ya mali zetu na waume zetu pia, Ni maombi pekee ndiyo
yanayofungua njia iliyonyooka kwa muombaji
Ezra 8:21 – 23, Hivyo usipuuze maombi mwana wa Mungu maana
utakapoomba kwa bidii utapewa sawa sawa na maombi na sio nje ya maombi, Zaburi
20:8, hivyo wamama wa injili kuweni kama wanawake wa Biblia ambao
waliomba pasipo kuchoka, nanyi mtavuna msipozimia roho maana maombi hayafi.
Katika
siku ya mwisho ya kongamano hilo Mchungaji Katunzi alihitimsha kwa maombi
maalumu ya Baraka za kifamilia na ulinzi wa ukuta wa moto ambapo alitamka
Baraka maalumu kwa wote waliofika katika kongamano hilo kwa kuwaombea ustawi wa
kiroho na kimwili pamoja na ustawi wa watoto wao na waume zao pia.
Wakizunguza
na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake waliofika katika kongamo
hilo wamesema kuwa hakika kongamano hili limekuwa la Baraka sana kwetu sisi
akina mama wa Mbeya kwani sasa Kanisa la mkoa wa Mbeya limepata nguvu mpya na
Ndoa zetu zimepo kabisa na watoto wetu nao wamepona na hata mali zetu pia zimepona
kwelikweli.
Naye
Mkurugenzi wa wamama wa jimbo la Mbeya Mama Mchungaji Mlawa amesema huu ni
wakati ambao Bwana Yesu alikuwa ameukusudia kwetu na hakika Mungu amemtumia
mchungaji Katunzi sawasawa na vile ambavyo sisi wamama tulimuomba Mungu ampe
Ujumbe Mchungaji Katunzi wakusema nasi wamama na kweli hii inadhirisha wazi
kongamo hili lilikuwa na nguvu zisizo za kawaida na Mungu ameongea nasi.
Aidha
kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa Kanisa EAGT Gilgali Mwanjelwa Makamu
Askofu Mkuu Dr. Asumwisye Mwaisabila yeye amasema kuwa Mchungaji Katunzi
amefanyika Baraka katika kongamano la wamama na hakika ameona Mungu akimtumia
kwa namna ya ajabu sana na akamuonya akisema kuwa kamwe asije akaacha injili
anayohubiri sasa kwani Bwana Yesu amemuitia injili hiyo, na mwisho Askofu Dr. Mwaisabila
akatoa nasaha zake akisema “Mwanangu
Katunzi huu si muda wa kusikiliza maneno
ya watu kwani hayana maana katika kazi Bwana wetu Yesu Kristo mimi Baba yako
Nakupenda sana furaha yangu ni wewe kusonga mbele, Na kama mimi Baba yako
ningelisikiliza Maneno ya watu nisingefika hapa nilipofika, hivyo Mwanangu Katunzi
songa mbele kwa kazi ya Bwana Yesu mimi ni Mzee sasa nataka twende Mbinguni
Kijana wangu ” hayo ni maneno ya
wosia ya Askofu Mwaisabila aliyoyatoa kwa mchungaji Katunzi ambapo watu wote
waliokuwepo ndani ya kongamano hilo walishindwa kujizuia na kupelekea kuangua
kilio kikubwa kilichotikisa kongamano zima kwa maneno mazito ya Mzee huyu.
Kwa
upande wake Mchungaji Katunzi yeye alifurahishwa kwa namna ambavyo Mungu
alivyoonekana katika wiki yote ya Kongamano la wamama na zaidi aliwashukuru
wamama wote wa Mji wa mbeya kwa namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe wake
wote,
“Kwa kweli ninyi akina mama mmekuwa chachu ya injili kila mahali injili
inapofika hakika ninyi ni jeshi kubwa sana, na kipekee nimshukuru Makamu Askofu
Mkuu Dr. Mwaisabila na Timu yake ya hapa Mbeya kwa kuweza kuratibu vema kongamano,kwa
ushirika mkuu na Ofisi ya Jimbo la Mbeya”
Mwisho
Mchungaji Katunzi alitoa Mchango wa Fedha shilingi laki tano kwa wamama wa
Jimbo la Mbeya ambayo aliwakabidhi viongozi wajimbo hilo kwa niaba ya wamama
wote, huku Madhabahu ya Kanisa la EAGT
Gilgali Mwanjelwa akiichangia kiasi cha Fedha Shilingi laki tano ambapo
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Makamu Askofu Mkuu Dr. Mwaisabila
alikabidhiwa na Mchungaji Katunzi.
Picha ya chini ni Mchungaji Athanase Camilly akifundisha katika kambi la wamama mjini Mbeya.
Akina Mama wakiomba kwa bidii katika kongamano laWWI Mbeya mjini.
Mchungaji Katunzi akitoa Mchango wa Shilingi laki tano kwa viongozi wa WWI Mbeya.
Mchungaji Katunzi akongoza Maombi kwa wamama pamoja na picha zinazofuata hapa chini.
Makamu wa Askofu Mkuu wa EAGT Dk. Asumwisye Mwaisabila akongea na Wamama.
Askofu Mwaisabila na Mchungaji Katunzi wakieleza jambo kwa pamoja katika Kongamano hilo.
Askofu Mwaisabila akimuombea Baraka Mchungaji Katunzi na Ulinzi wa Mungu.
Askofu Mwaisabila na Mchungaji Katunzi akikumbatiana kwa Furaha baada ya Kongamano kumalizika.
No comments:
Post a Comment