Akizungumza katika Ibada kuu ya Kanisa la City Center Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola amesema kuwa hakika huu ni wakati muhimu wa kuwaelezea juu ya imani potofu iliyoingia katika makanisa huku akikemea vikali Imani ya Mitume na Manabii.
Aidha amewataka waamini wote kuelekeza nguvu zao katika kusimamia maombi na kuacha kutegemea vitambaa na mafuta ya upako na vingine vinavyofanana na hivyo.
Katika Pichani baadhi ya Matukio yaliojiri katika ibada ya Kanisa la EAGT City Center lililoko viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zamani Sabasaba.
Picha ya Chini ni Mzee Kiongozi wa Kanisa la EAGT City Center Ndugu Alex Mmbaga akimpokea Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola baada ya kuwasili Kanisani hapo
Picha Juu ni Bahati Bukuku akiimba katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center wiki iliyopita ambapo Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola alikuwa Mhubiri wa Siku.
Askofu Mkuu Dkt. Moses Kuloa akimuombea Mzee Kiongozi Ndugu Alex Mmbaga kuanzisha Ujenzi wa Kanisa la EAGT City Center ambapo Ndugu Mmbaga ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
skofu Mkuu Dkt. Moses Kuloa akimuombea Mama Bokke kwa niaba ya Wanawake wote kuanzisha Ujenzi wa Kanisa la EAGT City Center ambapo Mama Bokke ni Mjumbe wa Kamati hiyo.
Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola akihubiri wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God City Center.
Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola akimuombea Mmoja wa Akina Mama wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God City Center.
skofu Mkuu Dkt. Moses Kulola akimuombea Mmoja wa Watoto wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God City Center.
No comments:
Post a Comment