Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amerejea Dar es Salaam mchana wa leo, Jumanne, baada ya kumaliza ziara
ya siku tisa katika mikoa minne ambako amekagua, kuanzisha ama kuzindua
miradi 19 ya maendeleo na kutembea kiasi cha kilomita 2,770.
Rais
Kikwete amewasili Dar es Salaam akitokea Dodoma ambako amefanya ziara
ya kikazi ya siku mbili baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.
Katika
Mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete alianzia ziara yake Oktoba 28,
mwaka huu, miongoni mwa mambo mengine alikagua nyumba za wahanga wa
maporomoko ya mwaka 2006 kwenye kijiji cha Goha na akafungua Kiwanda cha
Kusindika Tangawizi kilichoko Mamba Miamba, Wilaya ya Same, na
akafungua Shule ya Sekondari ya Kata ya Asha Rose Mingiro iliyoko mjini
Mwanga.
Miradi
mingine aliyoifungua Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro ni
uzinduzi wa barabara za Rombo Mkuu-Tarakea na Kwasadallah-Masama na
akafungua Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (NAO)
mjini Moshi.
Katika
Mkoa wa Arusha, Rais Kikwete alizindua Hospitali ya Wilaya ya Arusha ya
Olturumet, akazindua Mradi Mkubwa wa Uboreshaji wa Miji kwa kufungua
barabara za Jiji la Arusha, akazindua Jiji la Arusha, akafungua rasmi
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela na akatembelea
Kiwanda cha Nguo cha A-Z.
Kabla
ya kuondoka Mkoani Arusha, Rais Kikwete alifungua Shule ya Msingi ya
Sokoine na kuzindua ukarabati mkubwa wa Barabara ya Minjingu-Arusha.Mkoani
Manyara, Rais Kikwete alifungua rasmi Barabara ya
Singida-Minjingu-Arusha, akazindua mradi mkubwa wa maji wa Mji wa Babati
na akaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya Babati-Bonga.
Mkoani
Singida, Rais Kikwete alizindua mradi mkubwa wa maji wa Mwankoko kwa
ajili ya Mji wa Singida, akaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa
Barabara ya Manyoni-itigi-Chaya na akafungua Barabara ya Issuna-Manyoni.Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2012
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2012
No comments:
Post a Comment