Picha ya juu Mchungaji Dk. Ngaleni akimkaribisha Mhubiri wa Semina Mwinjilisti Kiungo tayari kwa Neno la Semina.
Picha ya juu ni Mwinjilisti Kiungo akisalimia Wanasemina Katika Kanisa la KKKT Kurasini hapo jana.
Picha ya juu ni Mwinjilisti Kiungo akiongoza kipindi cha kumuabudu Mungu kabla ya neno.
Picha ya juu ni baadhi ya Washiriki wa semina katika Kanisa la kurasini wakimuabudu Mungu kwa pamoja.
Picha ya juu ni baadhi ya washiriki waliofika kwenye semina wakimuabudu Mungu kabla yaNeno.
Picha ya juu ni Mchungaji Dk. Ngaleni akimuabudu Mungu kabla ya Neno la Mungu.
Picha ya juu ni Bango la kitambaa likionekana mbele ya Kanisa na Ujumbe wa Semina.
Picha ya juu ni baadhi ya waimbaji wakishiriki kwa pamoja katika kumuabudu Mungu.
Picha juu ni Mwinjilisti Kiungo akifungua kwa maombi semina ya Neno la Mungu yenye kichwa cha somo Mtakatifu ni Nani.
Hapa chini ni Mafundisho ya Semina ya leo.
MAMBO YA MUHIMU UKITAKA KUWA MTAKATIFU
Nini maana
ya utakatifu?
1. Utakatifu
maana yake ni kuwa mkamilifu.
Mt.5:48.
“Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama
Baba yenu wa Mbinguni alivyo makamilifu .”
Law.11:44; “ Kwakuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu;takaseni
nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwakuwa mimi ni mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu
kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya Nchi.”
Law. 19:2; “Nena na mkutano wote wa wana wa Israel,
uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA Mungu wenu, ni mtakatifu.”
Law. 20:7,26 “Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa
mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa
mimi BWANA ni mtakatifu, nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe
wangu.”
2. Mtu asiye na
hatia.
Efe.1:4
“Kama vile alivyo tuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu,
ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”
MAISHA YA
MWANADAMU KABLA YA DHAMBI
MWA. 2:4-18, 21-25 “ Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na Nchi hapa kuwa na
mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana
Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi. Ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu
ya uso wote wa ardhi. BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,
akampulizia puani pumzi ya uhai akawa
nafsi hai. BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka
ndani yake huyo mtu aliyemfanya. BWANA
Mungu akachipusha kila mti unaotamanika
kwa macho, na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa
ujuzi wa mema na mabaya. Ukatoka mto katika Edeni na kuitilia bustani maji na
kutokea hapo ukagawanyika ukawa vichwa vinne. Jina la wa kwanza ni Pishoni, na
ndio unaozunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu; na dhahabu ya nchi
ile ni njema;huko kuna bedola na vito Shoham.
Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
Na jina la mto wa tatu ni Hedekeli, ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wan
ne ni Frati. BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni
ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu akisema, matunda ya kila
mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku
utakapo kula matunda ya mti huo utakufa hakika. 18. BWANA Mungu akasema si vema
mtu huyo awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 21-25. BWANA
Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kasha akatwaa ubavu wake
mmoja kafunika nyama mahali pake. Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA
Mungu akaufanya mwanamke
ASILI
YA MWANADAMU MDHAMBI
Angalia
mwanzo wa dhambi ilivyoingia
sasa
uk ifika sura ya nne Adamu na mkewe wanaanza kupata watoto, wakiwa nje ya
bustani ya Edeni- angalia watoto wanazaliwa
Mwa. 3: 1-19,22-24- “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu
aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke,at! Hivi ndivyo alivyosema Mungu,
msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, matunda ya
miti ya bustani twaweza kula;lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani
Mungu amesema, msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke
hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayo kula matunda ya
mti huo, mtafumbuluwa macho, nanyi
mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti
wafaa kwa chakula wapendeza macho nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi
alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mmewe naye akala. Wakafumbuliwa
macho wote wawili wakajijua ya kuwa wa uchi wakashona majani ya mtini
wakajifanyia nguo. Kasha wakasikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini
wakati wa jua kupunga; Adam na mnkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA
Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adam akasema uko wapi? Akasema nalisikia sauti yako bustanini nikaogopa kwa
kuwa mimi ni uchi, nikajificha. Akasema ninani aliye kuambia ya kuwa uuchi? Je
umekula wewe matunda ya mti niyo kuagiza
usiyale? Adamu akasema huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja name ndiye aliyenipa
matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, nini hili
ulilolifanya? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya nikala. BWANA Mungu
akamwambia nyoka kwasababu umefanya hayo, umelaaniwa kuliko wanyama wote , na
kuliko hayawani wote walioko mwituni;
kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; name nitaweka
uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wake na uzao wako; huo utakuponda
kichwa na wewe utamponda kisigino.
Akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako;
kwa utungu utazaa watoto; na tama yako itakiwa kwa mmeo, naye atakutawala.
Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti
ambao nilikuagiza nikisema usiyale, ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, kwa
uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba
itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula
chakula, hata utakapo irudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u
m avumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”
,
roho ya ukaidi inaendelea- Kaini anamuua Abeli-wivu
Mwa.4:1-15 “Adamu akamjua mkewe naye akapata mimba, akazaa kaini akasema,
nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili.
Habili alikuwa mchunga kondoo, na kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye
Kaini akaleta mazao ya ardhi sadaka kwa
BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabari Habiri na
sadaka yake; bali kaini hakumtakabari wala sadaka yake. Kaini akagadhabika
sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, kwa nini unaghadhabu? Na
kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vema hutapata kibali?usipotenda
vyema dhambi iko, ina kuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa
uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, ( twende uwandani) ikawa walipo
kuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua. BWANA akamwambia Kaini yuko wapi Habili ndugu
yako? Sijui, mimi nimlinzi wa ndugu yangu? Akasema umefanya nini? Sauti ya damu
ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa umelaaniwa wewe katika
ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
utakapo ilima ardhi haitakupa mazao yake;
utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Kaini akamwambia BWANA,adhabu yangu
imenikulia kubwa haichukuliki. Tazama umenifukuza leo katika uso wa ardhi,
nitasitirika mbali na uso wako, name nitakuwa mtoro na mtu asiye kikao duniani,
hata itakuwa kila anionaye ataniua. BWANA akamwambia, kwa sababu hiyo yeyote
atakaye mwua Kaini atapatilizwa kisasi mara saba, BWANA akamtia Kaini alama mtu
amwonaye asije akampiga.”
-
mjukuu wa Kaini anaoa mitala kwa mara ya kwanza
Mstari wa 19 “ Lameki akajitwalia wake wawili; jina la wa kwanza ni Ada, na
jina la wa pili ni Sila.
Mstari wa 25-26-kwa mara ya kwanza watu walianza kuliitia jina la Bwana
Mwa. 5:24 – Hapa tena tuna muona Henoko anakwenda pamoja na Mungu
Mwa.
6-9- Mungu alichoka na maisha ya mwanadamu akaamua kuangamiza.
Huwo
wote ni mfululizo wa maisha ya watenda dhambi ndiyo sababu ya Daudi kusema
maneno yafuatayo
Zab. 51:5 “ Tazama,
mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama alinichukuwa mimba hatiani.”
Ayu. 14:4 “ Ninani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu
kichafu? Hapana awezaye.”
Rum.5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa
dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote
wamefanya dhambi.”
Mwa. 5:3 “ Adamu akaishi miaka mia
na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake , akamwita jina lake
Sethi.”
Nani
mtakatifu?
1Yoh. 1:8-9 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli
haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata
atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha
na udhalimu wote.”
Mith.28:13 “ Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na
kuziacha atapata rehema.”
MAMBO AMBAYO
NI LAZIMA UFANYE ILI UWE MTAKATIFU
KUZALIWA
MARA YA PILI
Yon. 3:1-6 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo, jina lake Nikodemo,
mkuu wa wayahudi. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u
mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hapana mtu awezaye kuzifanya ishara hizi
uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu akamwambia amini,
amini nakuambia, mtu asipo zaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Nikodemo akamwambia, awezaje, mtu kuzaliwa akiwa mzee? Awezaje kuingia tumboni
mwa mamaye mara ya pili , akazaliwa? Yesu akajibu amini, amini nakuambia mtu
asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa
kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”
Eze.36:25-27 “ Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi;
nitawatakaseni na uovu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Name nitawapa ninyi moyo mpya, name nitatia
roho mpya ndani yenu, name nitatoa moyo wa jiwe uliyomo ndani ya mwili mwenu,name nitawapa moyo wa nyama. Name
nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwa endesha katika sheria zangu, nanyi
mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”
Tit.3:5 “ Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyo yatenda sisi, bali kwa
rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho
Mtakatifu.”
KUSAMEHE
Mt.6:14-15 “ Kwa maana
mkiwasamehe watu makosa yao, na baba yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi. Bali
msipowasamehe watu makosa yao, wala baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Mk.11:25-26 “ Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni mkiwa na neno juu ya
mtu; ili na baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini
kama ninyi hamsamehe, wala baba yenu aliye mbinguni, hatawasamehe ninyi makosa
yenu.”
Mt.5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni na huku ukikumbuka kuwa
ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako
upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi utoe sadaka yako.”
KUTOA SADAKA
AINA ZA MATOLEO.
1 LIMBUKO (Malimbuko): Mith 3:9-10
v
Limbuko ni zao la kwanza
la kazi ya mikono yako. (First fruits)
· Kazi ya limbuko, ni
kumheshimu Mungu
3.
ZAKA ( FUNGU LA KUMI): Walawi
27:30, Malaki 3:7 – 7
Mwanzo wa
zaka
Zaka
ilianza zamani kabla Mungu hajaweka sheria ya watu kutoa zaka. Wako watu walio
mpenda Mungu kwa mioyo yao na walio mtolea Mungu bila kulazimishwa na sheria
ila walitoa kwa mioyo yako. Watu hawa walitoa aina hii ya sadaka ikamfurahisha
Mungu kiasi ambacho alivyo barikiwa nayo akaamua kuweka sheria ili vizazi vyote
duniani vifute sheria hii kwa ajili ya kujipatia Baraka. Angalia mifano
ifuatayo ni ya watu wa kwanza walio toa sadaka hii ya zaka kabla ya sheria ya
Musa.
v IBRAHIM
Mwa.14: 17-20
: “ Abrahamu aliporudi kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja
naye, mfale wa Sodoma akatoka amlaki katika Bonde la Shawe, nalo ni bonde la
mfalme. Na Melkizedeki mfalme wa Salem , akaleta mkate na divai, naye alikuwa
kuhani wa Mungu aliye juu sana.
Akambariki, akasema, Abrahamu na abarikiwe na Mungu aliye juu sana,
muumba mbingu na Nchi. Ahimidiwe Mungu
aliye juu sana, aliye watia adui zako
mikononi mwako. Abram akampa fungu la kumi la vitu vyote.”
v YAKOBO Mwa. 28: 20-22 “ Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu
akiwa pamoja name, akinilinda katika njia niiendayo na kunipa chakula nile, na
nguo nivae, name nikirudi kwa amani
nyumbani kwa Baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililo
lisimamisha katika nguzo litakuwa nyumba
ya Mungu wangu. Na katika kila utalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya
kumi.”
- Zaka ni 10%
(asilimia kumi) au 1/10 au sehemu moja kati ya kumi ya baraka yoyote aliyokupa
Mungu.
“lete zaka kamili nyumbani kwangu” (Malaki
3:10)
v Kazi ya zaka – ni kufungua madirisha
ya mbinguni ili baraka zimiminwe. Zaka
haipimi baraka (mavuno) bali inafungua madirisha ya mbinguni ili upimiwe baraka
kutoka kwenye matoleo ya sadaka yako baada ya zaka.
·
Endapo utazidiwa na matumizi, na ikakulazimu kuitumia zaka
takatifu ya Mungu, fahamu kwamba, Mungu anakudai. Siku utakapomrudishia, utatakiwa kulipa pamoja na riba, ili zaka
yako ikombolewe.
·
Kukombolewa maana yake ili iwe zaka takatifu
tena ni lazima uiongezee 20% au
1/5 (sehemu ya tano )ya hiyo zaka, iwe
kama riba, ndipo Mungu ataipokea kuwa ni zaka takatifu ya Bwana. Laa sivyo, zaka yako, si kamili, hivyo si
takatifu. Kwahiyo, haitafungua madirisha
ya mbinguni.
3.
DHABIHU (Sadaka ya kawaida) *2Kor 9:6-7
· Sadaka ya
dhabihu haina hesabu toka kwa Mungu, bali kila mtoaji, anaamua mwenyewe atoe
kiasi gani. Utakavyoamua ndivyo
utakavyovuna. Ukitoa kidogo,utavuna au
utapimiwa kidogo, ukitoa kwa wingi, utapimiwa vingi. Ni uamuzi wako. (Gal 6:7 – 10)
· Kazi ya Dhabihu: Ni kupima kiwango cha mavuno ya
baraka, unayotakiwa kumiminiwa kutoka mbinguni baada ya kutoa zaka.
UONGOZWE
NA ROHO MTAKATIFU
Mwa.
1:1-2 “ Hapo mwanzo Mungu aliziuumba mbingu na Nchi. Nayo Nchi ilikuwa ukiwa
tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu
ikatulia juu ya uso wa maji.”
Mdo.
1:8 “ Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi
mtakuwa mashaidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria,
na hata mwisho wa Nchi.”
Rum.8:1-11
“ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa
sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru,
mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyo dhaifu kwasababu ya mwili,
wangu, kwa kumtuma mwanawe mwenyewe
katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi
katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa
kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho. Kwa maana wale waufuatao mwili
huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa
ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala
haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili
hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi
hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho
wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa
ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu I hai kwa
sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliye mfufua Yesu katika wafu
anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili
yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anaye kaa ndani yenu.”
Kwa
hiyo ili mwadamu akamilike hatu tatu muhimu lazima zipitiwe
v MUNGU BABA-
yeye ndiye muumbaji -
lazima aumbe
v MUNGU MWANA-
yeye ndiye mkombozi - lazima
aokoe
v MUNGU ROHO
MTAKATIFU- yeye ni mtakatifu - lazima
atakase
BY
EV. TITUS G. KIUNGO (titus2tz@yahoo.co.tz)
facebook- titus kiungo
No comments:
Post a Comment