Dodoma.
Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania katika Mkoa wa Dodoma wilaya ya Kongwa limeendelea na Ujenzi wa Kanisa lake lililotumia Mpaka sasa Gharama ya shilingi milioni mia nne kwa kuwahimiza wapenda injili ndani ya Tanzania kuwekeza kwa Kristo kwani kufanya hivyo ni kuliinua jina la Bwana Yesu kwa njia ya utoaji.
Akizungumza na Mwandishi habari hii Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Dennis Livingstone amesema kwa sasa kanisa hilo limetumia kiasi cha shilingi za Kitanzania Mia nne katika ujenzi wa awali, huku ujenzi ukiwa bado unaendelea katika kanisa hilo lenye makao yake wilayani Kongwa.
Kanisa la EAG ( T ) lipo chini ya Mwinjilisti wa kimataifa na Mhubiri wa injili hapa Tanzania Dk. Moses Kulola ambaye ndiye Askofu Mkuu wake, hivi sasa Kanisa la EAGT limekuwa na mikakati mingi ya kuleta watu kwa Yesu kama misingi ya imani yake kuundwa mwaka 1992.
Katika Picha za chini ni Jengo linaloendelea kujengwa na waumini wa Kanisa hilo
Picha ya chini Jengo la zamani ambalo bado linatumika kwa Ibada.
No comments:
Post a Comment