Na Yonathan Landa.
Kanisa la Tanzania Assemblies Of
God Mkoa wa Mbeya limefanya Semina ya Nguvu za Mungu yenye kichwa cha somo WAZO
LA MUNGU kwa Ushirikiano wa Makanisa
matano kwa ajili ya kuharibu kazi za shetani mkoani hapo, Kanisa hilo ambalo ni
moja kati ya makanisa yaliyojitolea kupelekea injili ya Kristo Yesu mwana wa
Mungu kwa gharama wamefanya semina hiyo kuanzia siku ya Jumatano ya tarehe 11
July 2012 hadi siku ya Jumapili ya tarehe 15 July 2012 katika Kanisa la TAG –
Rehoboth International Christian Center (RICC) linaloongozwa na Mchungaji
Kiongozi Sunday Matondo ambaye ndiye aliyekuwa
mwenyeji wa Semina hiyo.
Semina hiyo ambayo ilihudhuriwa
na waumini mbalimbali kutoka makanisa mbalimbali hakika ilikuwa na nguvu za
Mungu zisizo za kawaida hasa kutokana na watumishi waliokuwa wakiendesha semina
hiyo kuwa na Nguvu za Mungu zisizo za kawaida.
Semina hiyo ilifundishwa na
wahubiri kutoka ndani ya nchi yetu ya Tanzania na kutoka nchi jirani ya Malawi
ambapo kutoka Tanzania Mchungaji Frolia Katunzi kutoka Kanisa la Evangelistic
Assemblies Of God Tanzania alifundisha na kutoka Malawi alifundisha Askofu na
Nabii Steven Mwila, huku wachungaji
wenyeji walioshiriki kuratibu semina nzima ni Mchungaji Lauden Mwafongo kutoka
TAG – Gilgali RRM na Mchungaji Imani Masiku kutoka TAG – Jorai Itunda.
Katika picha ni baadhi ya matukio yaliyoweza
kupatikana na Kamera yetu.
Picha ya Juu ni Baadhi ya Wachungaji washiriki katika Semina ya Wazo la Mungu.
Askofu na Mtume Steven Mwila na Mkewe wakifuatilia kwa makini wakati Mchungaji Katunzi alipokuwa akifundisha.
Meneja wa Radio Ushindi Mchungaji Mathew Sasali iliyoko Mkoani Mbeya akifuatilia kwa Makini mafundisho ya Wazo la Mungu.
Mchungaji Katunzi wa Kanisa la EAGT City Center akiendesha Maombi huku Mchungaji Sasali akiendesha Timu ya Kusifu na Kuabudu.
Mchungaji Mwenyeji Sunday Matondo na Askofu na Nabii Mwila wakiwa wamezama katika hali ya Maombi kwenye Semina ya Wazo la Mungu.
Mchungaji Athanase Camilly wa EAGT Issanga Mbeya akiwa amezama kwenye Maombi na wachungaji baadhi.
Haikuwa rahisi kwani hata waimbaji nao walizama katika hali ya Maombi kama unavyoowaona.
Picha tatu za Juu ni Mchungaji Katunzi akiendesha Maombi kwa baadhi ya washiriki wa semina ya Wazo la Mungu.
No comments:
Post a Comment