Picha ya juu, Mwenyekiti wa UWAKITA Mwinjilisti Samson Bullegi akitoa ufafanuzi juu ya Ubaguzi wa Jeshi la Polisi kwa Wakristo hapa Nchini
TAMKO LA
WAINJILISTI WA KIKRISTO TANZANIA
TAREHE 14
/06/2012 MKOANI DAR ES SALAAM
JIHAD YA
KUANGAMIZA UKRISTO SASA IMEPAMBA MOTO
Sisi, Umoja wa Wainjilisti Tanzania
tuliokutana hii leo kufuatia hali ya
machafuko na uchomaji wa Makanisa, vitisho dhidi ya Wakristo na mali zao huko
Zanzibar;
Tumekuwa tukitoa matamko ya tahadhari
kwa muda mrefu sasa, juu ya matamko yanayotolewa katika makongamano ya Waislamu
ambapo kwa kweli tunasikitika kuwa hatukusikilizwa ipasavyo na mamlaka husika.
Tulipofika kwenye awamu ya Pili ya
utawala wa Tanzania, pakazuka vikundi vya vijana wa Kiislamu. Vikundi hivi vilifanya
mikutano ya kuchambua na kukosoa Biblia, kama walivyotaka.
Ilivyoonekana vikundi hivi viliandaliwa
tangu siku nyingi vikisubiri tu atakapokuja Rais Mwislamu waanze kazi ya kuubomoa bomoa Ukristo na kuangamiza
Wakristo wenyewe. Sanjari na harakati hizo pakafanyika mipango ya siri ya
kuiingiza Zanzibar kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (O.I.C) na
pakatokea mapigo dhidi ya Kanisa kama ifuatavyo:-
HAPA TUNAORODHESHA MATUKIO
MACHACHE TU KUTHIBITISHA TUSEMAYO:-
1.
MWANZA: Mkristo mmoja akachomewa nguruwe wake
kwa moto wa Petrol na mali zake kuharibiwa na Waislamu.
.
2.
MAGOMENI:- Mkristo mmoja aitwaye Mbokomu alivunjiwa bucha zake za
nguruwe Manzese, huku wavunjaji wakipiga kelele za TAKBIR, wakiwa wamebeba nyundo na mashoka.
3.
TANGA:- Kantini ya Kanisa Katoliki ilichomwa moto na Waislamu.
4.
KIBAHA:- Kanisa la Kianglikana nalo lilichomwa moto.
5.
Mwaka
2002 Kanisa la African Inland (AICT) Pahi Wilayani Kondoa lilichomwa moto na
Waislamu na kuteketea.
6.
Mwaka
2003 Waislamu walivamia mhadhara wa Wakristo eneo la Kimara Baruti wakitokea
msikitini na kuharibu vyombo vya mahubiri hayo. Polisi, lakini hapakuwa na utekelezaji wowote pamoja
na kufuatwa mara kwa mara ili wachukue hatua lakini ikawa kimya.
7.
Tarehe 9 Novemba 2004, Waislamu wa Namanga kwa
kushirikiana na Wasomali kutoka nchi jirani ya Kenya walivamia mkutano wa
Injili huko Namanga na kuharibu mali. Jeshi la Polisi halikuchukua hatua
yoyote.
8.
Mwezi
Agosti 2007, Waislamu walivamia na walivuruga ibada ya Jumapili ambayo pia
ilihusisha ibada maalumu ya Sakramenti ya Kipaimara iliyokuwa inaendeshwa na
Askofu Gerald Mpango wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Western Tanganyika
huko Nguruka, Kasulu Mkoani Kigoma.
9.
Mwaka
2008 Waislamu walivamia mkutano wa Injili huko Kalya wilayani Kigoma Kusini na
kuharibu vyombo vya Kanisa vyenye thamani ya Dolla 8,000/=
10.
Tarehe
25 Februari, 2011 Waislamu katika mji
mdogo wa Mto wa Mbu walivamia mkutano wa Injili na Kuharibu mali za thamani
kubwa sana kujeruhi watu na hatimaye kusababisha kifo cha Mwinjilisti, Jackson John wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wilaya ya Monduli, Mto wa Mbu.
11.
Tarehe 21
Septemba 2011 kulitokea uchomaji wa makanisa (1)(TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD
(T.A.G)-LUMALA PARISH (2)TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD (T.A.G.)-NYAMANOLO PARISH
AND (3)PENTECOSTAL ASSEMBLIES OF GOD (P.A.G.)-PASIANSI PARISH, Jijini Mwanza,
Uliofanywa na Waislamu.
12.
Na hivi karibuni kumezuka tabia ya Jeshi la Polisi
kukamata Wakristo wanaochinja wanyama wao wenyewe kinyume cha Sheria kwa
shinikizo la Waislamu.
MPANGO WA UCHOMAJI
WA MAKANISA ZANZIBAR
Mipango na
mikakati ya uchomaji wa Makanisa, iliasisiwa mnamo tarehe 15/01/2011, pale
Mashekh wa Zanzibar kwa kushirikiana na Mashekh wa Tanzania bara pamoja na
waumini wao, walipokutana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee
kupanga kile walicho kiita uzinduzi wa Makongamano ya kupinga Mfumo Kristo.
S
Makongamano
hayo hadi sasa, yamefanyika karibu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani, ukiiacha mikoa hii mipya, iliyotangazwa hivi karibuni na Serikali,
kwa lengo la kupandikiza chuki dhidi ya Ukristo.
Katika uzinduzi wa jukwaa
la Katiba mmamo tarehe 6/01/2012, Mashekh hao walikutana tena katika ukumbi huo
huo ambapo pamoja na mambo mengine waliyo jadiliana, kulikuwa na kauli
iliyotoka kwa mmoja wa wakilishi wa Zanzibar, Shekh Azan Khalith aliyesema tunam nukuu. “Sisi kwa upande wetu Zanzibar tunasema
kufa kupona Katoliki litang’oka mizizi yake Tanzania. Kwa hivyo nawaambia Waislamu
wasiichukulie kauli ya yule kafir mkubwa
aliyesema tusichanganye dini na siasa.” mwisho wa kunukuu.
Aliyekuwa
mgeni wa Heshima katika uzinduzi wa jukwaa hilo, Sheikh NASORO MOHAMED MAJID akiwashajiisha Wazanzibar alisema: “msiwe
na wasiwasi, Waislamu kuna mambo mawili tu kule, ima ziwe Serikali tatu au
Muungano umevunjika. Zanzibar kuna kitu
ndani yake ndiyo maana inang’ang’aniwa na si kingine isipokuwa ni UKRISTO, ambao
wana uhakika Zanzibar ikijing’amua katika huu unaoitwa Muungano, basi Uislamu
utapata nguvu, ukishapata nguvu kule, huku Tanganyika maji yanateremka tu.
Basi
huo mfumo Kristo ukifanikiwa katika mambo mawili haya yaani (kuung’oa) Basi
Waislamu wa Tanganyika tumeshakomboka (kombolewa).”
Mwisho wa kunukuu.
Matokeo ya
utekelezaji wa kauli hizo ni uchomaji wa Makanisa unaoendelea sasa.
Kwa kauli
hiyo hatukubaliani na maneno yanayotolewa na viongozi wa Serikali na watu
wengine wenye nia ya kuficha ukweli wa mambo kwa kusema kuwa waliochoma
makanisa ni wahuni na wendawazimu.
Uchomaji wa makanisa katika nchi yetu
haukuanza tarehe 26 Mei 2012, umekuwepo hadi sasa kwa muda wa miaka 11 huko
Zanzibar, na mara zote tumekuwa tukielezwa kuwa wachomaji ni wendawazimu.
Swali
la kujiuliza ni kwa vipi wendawazimu hawa huona Makanisa tu na hawakosei hata
siku moja kuchoma misikiti?
Kutumika kwa Jeshi la Polisi katika
Jihad ya kuuangamiza Ukristo nchini
Tunaunga mkono tamko la Maaskofu wa Zanzibar la tarehe
30-05-2012 na Tamko la CCT ambapo
sehemu kubwa ya masikitiko yao, wameelekeza kwa vyombo vya usalama hasa Jeshi
la Polisi, katika tamko hilo wamefichua mambo makubwa ambapo walisema kumekuwa
na kauli zinazotolewa na askari Polisi wazawa wa Zanzibar kuwa wataunga mkono
vurugu kila zitakapo tokea pia wakabainisha wazi kuwa tangu uchomaji na hujuma
mbalimbali kwa Kanisa zilipoanza kutokea, wamekuwa wakivijulisha vyombo vya
dola lakini hakuna hatua zozote zilizokwisha chukuliwa.
Kauli hiyo ya Maaskofu inaungwa
mkono na Waziri mwenye dhamana na Jeshi
la Polisi ( Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) kwa kauli aliyonukuliwa na vyombo
vya habari akisema:
“Jumiki imekuwa ikiendesha mihadhara kinyume
cha Sheria lakini mikutano yake bado imekuwa ikilindwa na Polisi ili isifanyiwe
vurugu na watu wengine. Sikubaliani na vitendo vya Jumiki vya kuchochea
uvunjifu wa amani kwa mwaka mzima na nusu huku ikilindwa na Polisi vinginevyo
Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo la Tanzania, Said Mwema, na Kamishina Mkuu wake
wa Zanzibar Musa Ally Musa, wachukue hatua za kuwajibika wenyewe bila
kulazimishwa.”
Kwa kauli hizo hatuoni shaka yoyote
kuamini kuwa Jeshi la Polisi linatumika katika Jihad ya kuuangamiza Ukristo.
MAAZIMIO YETU
i Hatuna imani na Jeshi la Polisi kutokana na
madhila haya yanayotokea ambayo hayachukuliwi hatua katika wakati muafaka.
ii Tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kujenga na kulipa gharama za uharibifu wa mali za Kanisa na za wahanga
wengine.
iv Serikali kujibu hoja za Waislamu juu ya MFUMO KRISTO unao lalamikiwa na
Waislamu; Kwa kukaa kimya kunawafanya jamii ya Waislamu waamini kuwa madai yao ni sahihi.
v Serikali kuchukua hatua dhidi ya wale wote
waliohusika na uchomaji wa Makanisa na uharibifu wa mali; kwani tunaamini wanafahamika.
Kutochukuliwa hatua stahiki kuna wafanya wahalifu hao kujiona kana kwamba wao
ndio bora kuliko jamii ya watu wengine hapa nchini Tanzania, na hata kufikia
hatua ya kujichukulia hatua na kuharibu mali za wasio Waislamu na hata
kusababisha madhara ya kifo.
vi Tumefadhaishwa na hotuba ya mheshimwa Rais juu
ya matukio ya Zanzibar, hotuba ambayo ilionyesha kuwabembeleza walio sababisha
uchomaji wa Makanisa na kuwataka wafanye shughuli zao kwa misingi ya kuanzishwa
kwa kundi hilo, sisi tunaamini kuwa kundi hilo halisitahili tena kuitwa kundi
halali, ni matumaini yetu kuwa sasa mheshimiwa Rais atatafakari upya na
kuchukua hatua sitahiki juu ya kundi hilo.
Vii
Tunaitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokuwalazimisha watoto wa Ki-kristo
kusoma dini ya Kiislamu mashuleni, na badala yake wapewe haki yao ya kusoma somo
la dini yao (ya Kikristo), kama inavyo fanywa kwa Waislamu.
iv Mwisho, sisi kama Wakristo, kwa namna ya pekee tunawaomba Maaskofu,
Wachungaji na wengine wote wenye dhamana ya kuliongoza Kanisa la Mungu hapa
Tanzania, kuichukua kadhia hii kama changamoto kuwa haya yanayotokea sasa,
yanafunua kile kilichoko nyuma ya harakati za Waislamu kuishinikiza Serikali ya
Tanzania kujiunga katika O.I.C, na hata ile shauku yao ya kutaka kubadilisha
Katiba na sheria za nchi ili kutoa nafasi ya kuundwa Mahakama za Kadhi.
Viongozi
wa Kanisa la Tanzania ambao hatuna shaka wanao uelewa mkubwa katika kutafakari
na kuchambua mambo, wanalo jukumu na wajibu wa Kitume, Kinabii na Kichungaji,
kuwaelimisha Wakristo na wananchi wengine wote wenye mapenzi mema juu ya namna
iwapasavyo kuenenda katika misingi ya sheria, haki, imani, na zaidi ya yote
katika kumpendeza Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
Mwinjilisti Mwinjilisti
Samson Renatus Bullegi
Cesil Simbaulanga
Mwenyekiti - Uwakita
Katibu - Uwakita
+255 714 050
866
+255 789 606 070
Mwinjilisti
Daniel Mwankemwa
Makamu Mwenyekiti - Uwakita
+255 716 305 120
No comments:
Post a Comment