Siku ya Jumapili ya tarehe 22 July 2012 ilikuwako Ibada ya Saa ya Ushindi na Kufunguliwa ambapo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania, EAGT City Center, Frolian Josephat Katunzi aliongoza Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika ibada hiyo.
Katika Picha ni Baadhi ya Matukio yaliyotokea leo katika Ibada ya Kanisa hilo.
Picha ya Juu ni Waimbaji wa Kwaya ya Majestic wakiimba wimbo wa Mifupa katika kipindi cha Kusifu na kuabudu.
Picha ya juu ni Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhulia ibada ya EAGT City Center.
Picha ya juu ni Muimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Afande Manoti akiimba wimbo wa Tuli! tulia! tulia! Yesu Yupo!.
Picha ya Juu ni Muimbaji Kalala akiimba katika kipindi cha Sifa leo katika Ibada ya EAGT City Center.
Picha ya juu ni Mchungaji Yohana Mwegoha ambaye pia ni Mchungaji akiimba wimbo wa Siku za Mateso yangu zinahesabika.
Picha ya Juu ni Mchungaji Frolian Katunzi pamoja na Mkewe Mama Katunzi wakifuatilia kipindi cha sifa na kuabudu hii leo.
Picha ya juu ni Mchungaji Gecha kutoka katika Mkoa wa Mwanza Kanisa la EAGT akiombea waumini waliotoa Sadaka kanisani hapo.
Picha ya juu Mchungaji Katunzi na Mkewe wakimuombea Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika Katika ibada ya siku ya Jumapili hii leo.
Picha ya juu Mchungaji Katunzi akihubiri hii leo katika Ibada ya Saa ya Ushindi na Kufunguliwa wakati wa Majira ya Mchana.
Picha ya Juu ni Mchungaji katikati ya Mahubiri akitoa baadhi ya Mifano jinsi ya kukabilia na Adui shetani kwa njia ya Maombi.
No comments:
Post a Comment