KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Sunday, August 12, 2012

IBADA YA JUMAPILI 12 AUGUST 2012 KWA MCHUNGAJI KATUNZI

Mchungaji Frolian Katunzi hii leo ameendelea na Ibada ya nguvu katika Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania City Center lililoko Katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere zamani Sabasaba ambapo wengi wa waliohudhuria ibada hiyo wamefunguliwa kwa jina la Yesu Kristo.

Mchungaji Katunzi amesema kuwa Ibada ya Jumapili ijayo ya tarehe 19 August 2012 itakuwa ni Ibada ya Nguvu na maalumu kwa wale wote wenye kusumbuliwa na matatizo ya Kuolewa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja ni kupita kwa Umri na kuvunjika kwa Uchumba, hivyo Mchungaji Katunzi amewaomba wale wote wenye kusumbuliwa na Matatizo hayo wafike katika Kanisa la EAGT City Center.

Katika picha ni baadhi ya Matukio yaliyotendeka katika Ibada ya EAGT City Center.

 Picha ya juu ni Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.
 Picha ya juu ni Muimbaji wa nyimbo za Injili Lina Swai katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.
 Picha ya juu ni Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walioshiriki katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.
 Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akihubiri katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center Ibada iliyofanyika katika Ukumbi wa Sabasaba.
 Picha ya juu ni Baadhi ya mmoja kati ya wengi waliofika kufanyiwaMaombi katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.
 Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akiwafanyia Maombi baadhi ya Wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika kufanyiwaMaombi katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.
Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akiwafanyia Maombi baadhi ya Wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika kufanyiwaMaombi katika Ibada ya Kanisa la EAGT City Center kwa Mchungaji Katunzi.

1 comment:

  1. IMEKAA POUWA SANA IBADA HIYO LAKINI BOFYA NA HAPA www.jaizmelaleo.blogspot.com

    ReplyDelete