KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Sunday, February 26, 2012

IBADA YA USHINDI NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER



       Na: Mwandishi Wetu.
              Dar es Salaam.
Kanisa la Evangelist Assembies of God Tanzania ( EAGT) City Center Jijini Dar es Salaam chini ya Mchungaji Frolian Katunzi limeendesha Ibada ya Maombezi katika Kanisa hilo lililoko katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere zamani Sabasaba ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Akihubiri katika Ibada kuu ndani ya kanisa hilo Mchungaji Katunzi amesema umefika wa Wakristo wa Tanzania kuacha kulalamika juu ya hali ya Nchi yetu na badala yake wasimame katika zamu zao kama Wana wa Israel walivyoweza kuchukua hatua ya kufunga na Kuomba juu ya taifa la Tanzania.

Mchungaji Katunzi amesema Migomo na Maandamo yataendelea ndani ya Taifa letu endapo hatutaweza kuchukua hatua thabiti juu ya Vizazi vyetu na watoto wetu kwa maombi ya kufunga na kuomba, akifafanua ibadani hapo amesema, nanukuu "Mimi sipingi Maandamano hata kidogo bali ipo hatua ya kuchukua kwa sisi wakristo nayo ni kuandamana kwa mabango makubwa kwa Mungu kwa kutumia maombi huku wenzetu Wanaharakati na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiandamana kwa Kuieleza na kuishurutisha Serikali kusikia kwa Mengi yanayotokea!

Aidha Mchungaji Katunzi ameelezea zaidi Hali ya Matatizo mbalimbali juu ya Taifa na Matokeo ya Wakristo kutokuchukua zamu zao ambazo ni pamoja na kumsihi Mungu wa mbinguni kutuepusha na Majanga mbalimbali, kwani mpaka sasa kila Mtanzania ni shahidi wa mambo yote yanayosikika na yaliyokwisha kutokea.

Pichani : Mchungaji Frolian Katunzi aliyeshika kipaza sauti akiendesha ibada ya Maombi kwa baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada ya jumapili ya tarehe 26 February 2012

No comments:

Post a Comment