KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Monday, February 27, 2012

GOMBO TOURS NA SAFARI ZA MISRI NA ISRAEL

Na: Mwandishi Wetu.

Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Gombo tours iliyoko jijini Dar es Salaam amesema kuwa ziko safari za kwenda Israel na Misri kwa Mwezi Mei, July, September na Desember,
akizungumza na Mwandishi wa Habari hii Mkurugenzi wa Gombo Tours Bwana Willy Moses Kulola amefafanua kuwa kwa sasa Kampuni yake imekwisha fanya safari zipatazo tatu katika kipindi cha Mwezi September 2011 mpaka Mwezi wa February 2012,

Katika safari ya kwanza Msafara ulianzia katika Nchi ya Kihstoria ya Misri ambako wana wa Israel walikaa Utumwani kwa miaka Mia nne na ishirini ( GOSHENI ) na baada ya hapo msafara ulielekea katika Nchi takatifu ya Israel kupitia jangwani, njia waliopita wana wa Israel wakirudi nyumbani,


Aidha katika safari hiyo washiriki walijionea ukweli maandiko Matakatifu yaliyoandikwa katika Biblia , Bwana Willy Kulola amesema kwa sasa Kampuni yake imejipanga kuandaa safari za kisasa ambazo zitaongozwa na viongozi mbalimbali wa Makanisa akiwemo Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania Dr. Moses Kulola katika safari ya Mwezi September na Dicember.

Katika Picha ya Pamoja Baadhi ya washiriki wa Safari ya Kiibada wakiwa Gosheni Misri

No comments:

Post a Comment