Na Yonathan Landa.
Dar es Salaam.
Chama cha Wanachi CUF ( The Civic United Front ) kimezidi kumeguka na kuonyesha nyufa zake kwa Taifa baada ya Idadi ya wanachama wake wanaojiengua katika chama hicho kuongezeka, mpaka sasa wanachama wa chama cha CUF wamezidi kuwa na hali ya sintofahamu katika mzozo wa Mbunge wa Wawi kupitia chama hicho Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya umoja wa Kitaifa Mheshimiwa Seif Sharif Hamad.
Mpaka sasa idadi ya wanachama waliojiengua kutoka chama hicho ni elfu nne na mia sita ( 4600) ambapo idadi ya walitoka chama cha CUF inazidi kuongezeka kila siku, akizungumza nami kwa njia simu Mheshimiwa Hassan Doyo amesema kuwa iko idadi nyingine ya wanachama wanaoendelea kujiengua kwa kila siku na bado idadi hiyo wanaendelea kuikusanya katika mikoa mingine.
Toka msuguano wa Hamad Rashid na Maalim Seif uanze kumekuwa na mazungumzo mengi hasa katika jamii juu ya Mtafaruku huu wakieleza kutokufurahishwa kwa utaratibu uliomo ndani ya chama hiko kilicho na nguvu visiwani Nzazibar, mpaka sasa Mkoa wa Mwanza wanachama wa CUF waliojiengua ni Elfu moja mia tatu ( 1300 ), Mkoa wa Tanga Elfu moja na mia nane ( 1800 ) na katika Mkoa Dar es Salaam waliojiengua wakiwa ni Elfu moja na mia tatu (1300 ).
Wiki hii pia Mzimu wa Hamad Rashid umezidi kukiandama chama hicho kwa idadi kuongezeka, tarehe 26 February 2012 waliojiengua CUF ni pamoja na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama hiko Mheshimiwa Kadawi Lucas Limbu, Mh. Limbu katika kuzunguzia kwake nini kilicho sababishha yeye kujiengua na wanachama wengine wenye nguvu ya ushawishhi katika Jiji la Dar es Salaam, amesema kwa sasa chama kimekwishavurugwa na viongozi Madicteta na wasiotaka kuambiwa ukweli na hakiwezi tena kurudi katika misingi ya Demokrasia kama awali kwa kutokukubaliana ndani ya vikao kwa misingi ya hoja za mabadiliko.
Mpaka
sasa tayari Chama kipya cha Alliance for Democratic Change ( ADC ) DIRA
YA MABADILIKO kimeanza kwa kupeleka rasimu ya mabadiliko kwa Msajili wa
vyama vya Siasa Tanzania ambamo viongozi wake ni wale waliojiengua
chama cha CUF, Mwenyekiti taifa wa Muda ni Said Miraji Abdalah na Katibu
Mkuu taifa ni Kadawi Lucas Limbu
Picha ya juu Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change ADC Mheshimiwa Kadawi Lucas Limbu
No comments:
Post a Comment