Na Yonathan Landa.
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya GOJAC GENERAL SUPPLIES LTD Bwana Jasper Monyo tarehe 20 February 2012 alivamiwa Ofisini kwake Mivinjeni Barabara ya Kilwa na majambazi wenye Silaha aina ya Bastola na Kuibiwa kiasi cha fedha taslim Shilingi Milioni Kumi na moja na magari Mawili ya aina ya Toyota Harrier na jingine aina Toyota Voxy yote yenye thamani ya shilingi Milioni arobaini na tatu.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa Bwana Monyo amesema majambazi hayo yaliingia kwenye Ofisi yake kama wateja waliokuwa wakikagua magari kwa lengo la kununua kama ilivyo kawaida na desturi ya wateja wenginge ilivyo katika ofisi yake, amesema ghafla wakati wakiwa katika ofisi yake majambazi wawili walimtolea Bastola kila mmoja na kumuamuru atulie kimya kwani wao walikuwa kazini, ambapo mmoja wao alimuamuru bwana Monyo kutaja majina ya wafanyakazi waliokuwepo kwa wakati huo na ndipo jambazi huyo alipowaita wafanyakazi hao mmoja baada ya mwingine.
Bwana Monyo amesema wakati wakiendelea kutafakari nini wafanye katika kujikwamua na kuweza kutoka mikononi mwa Majambazi hayo, ghafla yeye na wanyakazi wake waliamliwa kulala chini kisha walifungwa kamba mikononi na pingu za plastic miguuni kwa lengo la kutoweza kufanya lolote, pia janga hili liliweza kuwakuta wateja waliofika ofisini hapo kwa huduma mbalimbali baada hapo walidai fedha na funguo za magari mawili.
Aidha katika sakata hilo mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya GOJAC Bwana Ayoub Kigodi amesema kuwa amepata wakati mgumu sana kutokana na yeye kutaka kubishana na Majambazi hayo, baada ya Majambazi kudai Pesa na Funguo, kwani mzozo huo ulifikia hatua ya majambazi kutaka kunifyatulia Risasi.
Askari wa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road waliweza kufika katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada lakini walipofika majambazi hayo yalikuwa tayari yamekimbia na Mali walizuchukua.
Askari wa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road waliweza kufika katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada lakini walipofika majambazi hayo yalikuwa tayari yamekimbia na Mali walizuchukua.
Picha ya Kwanza kabisa Mkurugenzi wa GOJAC GENERAL SUPPLIES LTD Bwana Jasper Monyo akiwa Ofisini kwake Mivinjeni jirani na Benedictine Father s,
Picha Mbili za Juu ni Baadhi ya Magari yanayouzwa na Kampuni ya GOJAC GENERAL SUPPLIES LTD
No comments:
Post a Comment