Hii leo katika Kanisa la EAGT City Center kulikuwa na Ibada ya aina yake pale wakazi wa jiji la Dar es Salaam walipopokea Injili ya Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye Hai ilipohubiriwa na Mchungaji Frolian Katunzi kwa pamoja na Mchungaji Athanase Camilly walipohubiri kwa Pamoja katika ibada ya leo kanisani hapo.
Wakihubiri kwa pamoja kwa upako wa nguvu za Mungu watumishi hao wamempondaponda shetani isivyo kawaida, Kanisa hilo limemaliza kipindi chake cha Miezi kadhaa katika Ukumbi wa Bandari uliopo maeneo ya tandika na kuanzia siku ya jumatano hii na kuendelea wanarudi katika kambi yao ya muda mrefu katika viwanja vya maonesho vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere zamani Sabasaba.
Katika picha ni baadhi ya matukio yaliyojiri kanisani hapo.
Picha ya juu ni Mwalimu Peter Primo wa Kanisa la EAGT City Center akifundisha Kanisani hapo hii leo kabla ya Ibada kuu kuanza.
Picha ya juu ni baadhi Waimbaji wakioongozwa na Muimbaji wa nyimbo za Injili Bi Qeen Mchomvu Kuabudu katika ibada ya leo.
Picha ya Juu ni Mchungaji Frolian Katunzi akiongoza Maombi ya Asubuhi kabla ya Ibada kuu huku Timu ya waimbaji wakimsindikiza kwa kuimba nyimbo ya kuabudu kwa hisi kali.
Picha ya Juu ni Muimbaji wa nyimbo za Injili Victoria Simbeye akiimba nyimbo ya Kusifu hii leo katika ibada ya EAGT City Center.
Picha ya juu ni Mchungaji Athanase Camilly wa EAGT Isanga Mbeya akihubiri Injili ya Kristo Yesu mwana wa Mungu katika Kanisa la EAGT City Center hii leo.
Picha ya juu ni Mchungaji Athanase Camilly wa EAGT Isanga Mbeya akihubiri Injili ya Kristo Yesu mwana wa Mungu katika Kanisa la EAGT City Center hii leo.
Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi na Mchungaji Camillly kwa pamoja wakihubiri kwa pamoja mbapo injili hiyo iliitwa Two in One kwa mujibu wa Mchungaji Katunzi.
Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akihubiri Injili ya Kristo Yesu kwa Hisia kali leo katika kanisani EAGT City Center.
Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akihubiri Injili ya Kristo Yesu kwa Hisia kali leo katika kanisani EAGT City Center.
Picha ya Juu ni Timu ya Radio Wapo wakiongozwa na Bi Angelina Lukindo aliyeshikilia Kipaza Sauti.
Picha ya juu ni Watenda Kazi wa Kanisa la EAGT City Center wakitoa huduma ya maombi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hii leo.
Picha ya juu ni Mchungaji Katunzi akimuombea Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika katika Kanisa la EAGT City Center.
Picha ya juu ni Mchungaji Camilly akimuombea mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika katika Kanisa la EAGT City Center hii leo.
No comments:
Post a Comment