KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Thursday, July 5, 2012

ILIVYOKUWA JANGWANI JUMAPILI NA MOSES KULOLA

Siku ya Mkutano wa Injili ya mwisho katika viwanja vya Jangwani siku ya jumapili ya tarehe 01 July 2012 hakika ilikuwa si siku ya kila mtu kukosa kwani wengi walifunguliwa na vifungo vilivyokuwa vinawatesa.

Aidha waimbaji mbalimbali walikuwepo kwa kuhitimisha mkutano huo uliokuwa umejaa watu wa jiji la Dae es salaam wakiongozwa na Rose Muhando, Frola Mbasha, Martha Baraka, Christina Mbilinyi na waimbaji wengine wengi.

Katika picha ni baadhi ya Matukio yalikuwa katika Mkutano huo wa Jumapili wa tarehe 01 July 2012.

 Picha ya juu Askofu Kulola akimuwekea Mkono wa Baraka Askofu Gamanywa wa Huduma ya BCIC katika hadhara ya Jangwani siku ya Jumapili 01 July 2012
 Picha ya Juu Akofu Gamanywa wa Huduma ya BCIC akimshukuru Mungu kwa tendo la yeye kukutanishwa kwa Mara nyingine tena na Baba yake Askofu Mkuu wa EAGT Dr. Moses Kulola.
 Picha ya Juu Askofu wa Jimbo la Temeke EAGT Dr. Bruno Mwakibolwa akikumbatiana na Askofu Gamanywa baada ya Kutoa neno la shukrani katika viwanja vya Jangwani.
 Askofu Gamanywa akisalimia umati wa watu waliofika katika Viwanja vya Jangwani siku ya kuhitimisha Mkutano huo Jumapili ya tarehe 01 July 2012.

 Picha za juu zinazofuatana ni Muimbaji Bi Christina Mbilinyi akiwashirikisha Baraka za Mungu katika njia ya Uimbaji katika viwanjwa vya Jangwani.
 Picha ya Juu Muimbaji Martha Baraka akiwashirikisha Maelfu ya watu waliofika katika viwanja vya Jangwani Jina la Yesu.

 Picha za Juu ni Bi Rose Muhando akiwashirikisha Maelfu ya watu Utamu wa Yesu kwa jijini la Dar es Salaam jangwani siku ya Jumapili ya tarehe 01 July 2012.

No comments:

Post a Comment