Na Gazaeti la Kiongozi.
Askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Dodoma mhashamu Mathias Isuja
amewataka watawa na waamini kwa jumla, kushikilia imani yao na kulinda
huku wakimshuhudia Yesu hata kama wanakumbana na vikwazo
vinavyowawezesha kukatwa shingo kwani wao ni wafiadini duniani wenye
tunu mbinguni.
Amesema maisha ya utawa ni kufia dunia na kuishi hai kimungu hivyo,
lazima waamini wakiwamo watawa kukubali kufia dunia kwa kujikatalia
kila kitu na kujitwika msalaba na hatimaye kumfuata Kristo. Askofu
amesema hayo wakati akitoa salamu baada ya ibada ya jubilei ya miaka 25
na 50 ya masista wa shirika la mtakatifu jimboni Kondoa na kusisitiza
kuwa, waamini wanapaswa kuona fahari ya msalaba kwakuwa ndani yake, kuna
wokovu na raha ya milele.....
Askofu mstaafu Mathias Isuja akiwa na waziri mkuu mh. Mizengo Pinda.
No comments:
Post a Comment