KWA MAOMBI NA USHAURI WASILIANA NASI KWA SIMU: +255 718 267 171 / +255 784 367 826 au +255 754 367 826. P.O.Box 71415 KARIBU SANA.

Friday, September 21, 2012

WAUMINI WA KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA MASHARIKI KUKUTANA KESHO KUTATUA MIGOGORO

Na Yonathan Landa

Hapo kesho kuanzia majira ya saa 6 mchana kunatarajiwa kufanyika mkutano mkubwa wa waumini wa kanisa la Moravian ambao utakuwa na lengo la kujadili hali ya sintofahamu inayoendelea ndani ya jimbo la mashariki( jijini Dar es salaam na Pwani) ambako siku za hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa na vyombo vya habati nchini kuhusiana na mgogoro mzito unaoendelea ndani ya jimbo hilo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika usharika wa Tabata jijini Dar es salaam, katika tangazo lililosikika katika kituo cha Wapo Radio Fm tangazo hilo, linaeleza waliohitisha mkutano huo ni umoja wa mabaraza ya wazee na wakristo wa jimbo hilo likieleza agenda kuu ikiwa ni hatima ya halmashauri ya jimbo la mashariki baada ya kutokutana na maaskofu wa kanisa hilo na kutokupokea ushauri wao.Ambapo tangazo hilo likaenda mbali zaidi kwakusema hatima ya kanisa itatolewa hapo.

Jimbo la mashariki limekuwa katika mgogoro kwa muda mrefu sasa huku chanzo kikitajwa kuwa ni baina ya viongozi wa jimbo hilo ambapo licha ya juhudi za kutaka kumaliza matatizo hayo kufanywa inadaiwa kuna wasiokubali kusameheana, kikao cha kesho kinatarajiwa kuvuta waumini wengi zaidi wa jimbo hilo kujua yaliyomo ndani ya kanisa lao na hatima ya mgogoro huo kwa ujumla.

Maombi yako yanahitajika kwa ajili ya kikao hicho ili Mungu aingilie kati na mambo yakae sawa.


Askofu Alinikisa Cheyo wa kanisa la Moravian.

No comments:

Post a Comment