Hii leo Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Saalam wameandamana kutoka katika Ofisi ya Chanel Ten alipokuwa anafanya kazi Mwandishi Daud Mwangosi hadi katika viwanja vya Jangwani kwa lengo la kuieleza Serikali kutokufurahishwa kwa Mauaji ya Kinyama kwa Mwandishi Mwangosi Mkoani Iringa wiki iliyopita.
Katika Maandamano hayo yaliyoishia viwanja vya Jangwani yaliingia Dosari baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Dk. Emmanuel Nchimbi kuwasili pasipo mualiko kutoka kwa Wanahabari hao, ambapo hata hivyo Waziri huyo alikubari kusikiliza wazo la waandishi kumtaka aondoke eneo la tukio kwa kuwaacha wandishi waendelee na Ratiba waliyokuwa wameipanga.
Katika picha ni baadhi ya Matukio yaliyokuwa yamejiri hii leo
Katika Picha ni Baadhi ya Matukio yaliyokuwa yamejiri hii leo.
No comments:
Post a Comment