Kanisa lililochomwa huko Kigoma (Picha kwa hisani ya mtandao wa IPP) |
Hili ni kanisa ambalo lipo nje ya mkoa wa Dar es Salaam jambo linalolitia hofu huenda chuki za kidini na uchomaji wa makanisa ukazidi kuenea nchini Tanzania Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Buronge mjini Kigoma.
Kashai alisema kanisa hilo lilichomwa na watu wasiojulikana na kwamba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1,337,000 ziliteketea.
Alisema sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa huku upelelezi wa tukio hili ukiendelea ili kuwabaini wahalifu hao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment