Makamu
wa Rais, Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja ya tuzo ya
mshindi wa jumla kitaifa wa mlipa kodi hapa nchini, Afisa Mtendaji Mkuu
wa benki ya NMB, Mark Wiessing kwenye hafla ya 6 ya Siku ya Mlipa Kodi
jijini Dar es Salaam jana.
Afisa
Mkuu wa fedha wa benki ya NMB, Bw.Waziri Barnabas akiwa amebeba moja ya
tuzo zilizokakabidhiwa kwa benki NMB baada ya kuibuka mshindi katika
Siku ya Mlipa Kodi nchini. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam
jana. NMB ilikabidhiwa tuzo ya mshindi wa jumla kitaifa wa mlipa kodi,
mshindi wa pili katika taasisi za fedha na mshindi wa pili katika kundi
la walipa kodi wakuu nchini.
Makamu
wa Rais, Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto kwake), Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing (Wa kwanza Kulia) , Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Wa pili kushoto) Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (kushoto) na
washindi kumi bora wa siku ya mlipa kodi nchini.
No comments:
Post a Comment